Saturday 26 April 2008

Wanaanza kuanguka, mmoja baada ya mwingine.

Alianza Edward Lowassa, akafuata Ibrahim Msabaha, na muda haukupita, Nazir Karamagi akaaachia ngazi.

Kwa kasi hii, tunaweza kufika mwaka 2010 ikawa hatuna kiongozi hata mmoja ambaye hajaguswa na Kiwanda cha Kashfa cha Tanzania (KKT).

Niliwahi kutabiri, bila kuwa na ushahidi madhubuti, kuwa itakapofika 2015 Tanzania itakuwa na nafasi ya kupata Rais safi, ambaye hana kashfa wala marafiki wenye kashfa, na ambaye hataogopa kuchukuwa hatua dhidi ya wale wenye tuhuma za kashfa.

2 comments:

Anonymous said...

Haondoki mtu hapa! CCM itatawala mpaka ichoke.

Anonymous said...

Serikali ya Kikwete ina matatizo mengi. Lakini pamoja na hayo tujiulize: atakaposimama tena 2010 dhidi ya Mrema, Lipumba, Mbowe (au ni Zitto Kabwe, Chacha Wangwe, au Dk. Slaa?) atachaguliwa huyu huyu ambaye tunayafahamu matatizo yake, au tujaribishe wengine ambao watayafanya matatizo ya Kikwete kuwa mchezo wa watoto?

Tukumbuke sasa hivi Mzee Mwinyi, ambaye kuna wakati nae alionekana kiongozi dhaifu, anaonekana afadhali kwa mbali tu akilinganishwa na Kikwete.